Wilayani Kishapu Kukutana na Wadau

MoMECa watembelea Kishapu na kukutana na wadau

Taasisi ya Dr Monica Mhoja Edutainment Centre MoMEC, ilitembelea Kishapu tarehe 13/01/2017 na kuonana na Afisa Maedeleo wa Mkoa na kuitambulisha MoMEC na lengo la kutafuta watoto-wajane ili waweze kuwasomesha katika shule ya AGAPE. Walitoa nakala ya filamu fupi ya SAUTI YA KUNESE ili iweze kutumika kuoneshwa katika mafunzo au makundi mbalimbali katika kuhamasiha. Afisa Maedeleo alilipokea jambo hili kwa furaha na akasema kwa usitawi wa watoto hawa waliosahaulika, yeye kama mwakilishi wa Serikali atakuwa bega kwa bega kufanya kazi na MoMEC na wadau wake PACESHI na AGAPE.

MoMEC pia waliweza kuonana na Mwenyekiti wa Mtaa wa Kishapu Matanda na Mwenyekiti wa Kijiji na kutoa nakala ya Kunese ili kuweza kuoneshwa kwa viongozi wengine, wanakijiji na taasisi za dini.

PICHA MBALIMBALI ZA MATUKIO KISHAPU

Tuko Wilayani Kishapu tukifuatilia Watoto-wajane ili waweze kurudi shule tutawasaidia ada pale AGAPE. Afisa Maendeleo ya Jamii Kishapu akisikiliza kwa makini na tutasaidiana bega kwa bega pamoja na wenyeviti wa mitaa/vijiji na watendaji. Mungu bariki Kishapu. Mungu bariki Shinyanga. Mungu bariki Tanzania

Featured Posts
Recent Posts
Archive

FOLLOW US

​​Call us:

(+255) 0748080423

Email us:​​

momeccentre1@gmail.com

Find us: 

MoMEC Centre

C/O PO Box 65413

Dar es Salaam, TANZANIA

© 2020 MoMEC Centre

Proudly created by

Dr. Barry Emerson &

Cora Deacon 

  • Instagram
  • Facebook Social Icon
  • Twitter Social Icon
  • YouTube Social  Icon

momeccentre

momec

momec_centre

momec centre

This site was designed with the
.com
website builder. Create your website today.
Start Now