Ndoa za watoto ni ndoa ambazo zinafanyika kwa watoto kabla hawajafikia umri wa miaka kumi na nane.  Ndoa hizi hutokea kwa watoto wa kike na wa kiume lakini wanaoathirika zaidi ni watoto wa kike.  Ndoa za utotoni zinaweza kuleta madhara makubwa na kukosa haki za msingi kwa mtoto wa kike kama kukosa elimu, afya duni n.k.  Ndoa za utotoni zimekuwa nyingi sana Tanzania, mkoa wa Shinyanga unaogoza kwa kuwa na asilimia 59% ya ndoa za utotoni.

      Aliolewa akiwa na miaka 13

"Niliolewa na kuacha shule na ndipo mateso ya vipigo yalipoanza."

Aliolewa akiwa na miaka 14

"Baba yangu alinilazimisha kuolewa nikiwa na miaka 14, mume wangu alikuwa na miaka 36."
 

Shuhuda hizi ni za kweli zilizosimuliwa ama na wahanga wa ndoa za utotoni wa washirika wenzetu Agape Shinyanga, au zilizotokana na utafiti uliofanyika. Majina na picha sio za kwao ili kuwalinda.