Machapisho

Maono Yetu

Kuwa na jamii inayoheshimu haki za binadamu na kutokuwa na ubaguzi wa kijinsia.

Kuhusu sisi

 

MoMEC ni taasisi isiyo ya kiserikali, inayoedeshwa kwa kujitolea, yenye wasanii na  wanaharakati wanaotumia sanaa (kuelimisha na kuburudisha) kujengea watu uwezo kuelewa masuala ya sheria na haki za binadamu na kupinga ukatili wa kijinsia.

 

Mwanzilishi wake Dkt Monica Magoke-Mhoja ni mwanasheria na mwanaharakati wa haki za binadamu. Amekuwa akitetea haki za wanawake na watoto Afrika Mashariki hususan Tanzania na Uingereza. Baada ya masomo yake alianzisha shirika la Children’s Dignity Forum (CDF) kutekeleza yale aliyofanyia utafiti katika shahada yake ya uzamili, huo ulikuwa mwaka 2006.   Hata hivyo, baada ya kuona kuna umuhimu sana wa kutumia sanaa kuelimisha na kuleta mabadiliko, mwaka 2014 alianzisha MoMEC ili kujikita katika kutumia sanaa kuburudisha na kuelimisha ili kuleta mabadiliko kuodokana na mila zilizopitwa na wakati na zinazogandamiza. 

 

Kwa miaka mitatu ya mwanzo, MoMEC imejikita katika kutokomeza ndoa za utotoni na madhara yake na kuwapa watoto sauti. Utafiti unaonesha kwamba asilimia 37 ya vijana wa kati ya miaka 20-24 wameolewa wakiwa hawajafikisha miaka 18.

 

MoMEC kwa sasa inalenga kusaidia wahanga wa ndoa za utotoni kwa kuanzia mkoani Shinyanga ambao ndio unaogoza kwa ndoa na mimba za utotoni.  MoMEC inashirikiana na Kituo cha Wasaidizi wa Haki za Kisheria Shinyanga (PACESHI) katika kupinga ukatili wa kijinsia na ndoa za utotoni kutumia sanaa, kwa kushirikiana na kikundi chao cha maigizo.  Pia inashirikiana na Agape Aids Control Programme (AACP) ambao wana uzoefu katika kutumia sanaa kwa njia ya filamu kuibua matatizo ya ukatili wa kijinsia hususan ndoa za watoto.  Pia AACP ina kituo cha shule ya kujisomea kufanya mtihani wa kidato cha pili na cha nne.  MoMEC inasaidia wahanga wa ndoa za utotoni kurudi shuleni kutokana na michango mbalimbali kutoka kwa wadau.  Pia, na sehemu ya faida ya mauzo ya filamu kama 'Chozi la Binti Kibena' inayosambazwa na kampuni ya MOMEC Edutainment Center Ltd – MOMEC Production.  Ili kujua zaidi kuhusu wabia wetu Agape na shule wanayoendesha, angalia kwenye taarifa zetu hapa bofya hapa.

 

Ili kuhakikisha shirika linadumu na kuwa endelevu, mwaka 2015 ilianzishwa kampuni ya kujitegemea MoMEC Edutainment Center Ltd (certificate incorporation No. 119002) ikiwa na kitengo cha MOMEC Production yenye lengo la kutengeneza na kusambaza kazi za taasisi ya MOMEC na kutoa faida kusaidia taasisi ya MoMEC isimame na kutoa huduma kwa jamii.  Sehemu kubwa ya faida inakwenda kusaidia watoto walioachishwa shule wakalazimishwa kuolewa, au kutelekezwa au kufiwa na wanataka kurudi shule.  Kituo cha MoMEC kinashirikiana na asasi zisiso za kiserikali za AACP na PACESHI. 

 

Ili kuweza kuona kwa mapana zaidi athari za ndoa za utotoni na madhara yake kwa watoto, bofya hapa kujua juu ya wahanga wa ndoa za utotoni wanaosoma Agape kituoni na kusaidiwa na MoMEC.

 

 

Wabia Wetu 

Dr. Monica Magoke-Mhoja

Mwanzilishi na Mkurugenzi

 

Maadili

Usawa

Uwazi
Uwajibikaji
 

AGAPE AIDS CONTROL PORGRAMME (AACP)

P.O.BOX 2189, SHINYANGA.

Website:    www.envaya.org/aacp/

Barua pepe: agapeshy07@yahoo.com 

PARALEGAL AID CENTER SHINYANGA (PACESHI)

P.O.BOX 2202 – SHINYANGA

 

Barua pepeparalegal_aidcentreshinyanga@yahoo.co.uk

 

MoMEC PRODUCTIONS Ltd.

Certificate Incorporation No. 119002

P.O.BOX 65413, DAR ES SALAAM

Barua pepe: drmomec2014@gmail.com